Voice of Maasai - Kwata Fagio

Tushirikiane sote tuwe wamoja
Tushirikiane sote tuwe wamoja

Kwata fagio
natujali mazingira
usafi ndo leo

Mazingira yetu yana mpambano
Ukitaka kuyatunza sharti upambane
Usipende lala na miguu kutundika juu
Tufanye kazi mazingira yawe hali ya juu

Tupende majukum tusipatwe na magumu
Tushike na madumu, tukanyweshe mpaka juu

Mimina mimina mina weka maji
Tukanyweshe mazingira miti ipande juu
Mimina mimina mina weka maji
Tukanyweshe mazingira Maua yapande juu

Tushike madu twende mpaka majuu,
Tupande migomba tule mandizi madu
Tushike majukum, tusukume gurudum
Tusafishe mazingira maisha yasiwe magumu Mazingira yetu ni mazuri sana

Kwata fagio

Tujithamini, tusafishe mazingira
Uchafu wa nini, twasababisha umasikini
Usipitwe na rai, hebu fanya maamuzi
Usafi wa mazingira ni muhimu kwa afya yako Sote tuungane kwa pamoja Tuyapende mazingira yetu

Kamata kamata fagio safisha
Ukifyeka majani takataka we
Kamata kamata fagio safisha
Usitupe takataka wakitupa we
Kamata kamata fagio safisha

Wakamatwe wanaochafua mazingira yetu wakamatwe wasafishe wapande miti
Wakamatwe wanaochafua mazingira yetu wakamatwe Wasafishe wapande maua
Tukiyatuz mazingira yatatutunza
Tukiyaweka safi na wengine watajifunza
Pakiwa na mavumbi na wengine wapata funza
Tukiyalinda vyema na
Mungu atatukuzwa
Mazingira yetu ni uhai wetu sote

Kwata fagio

Tushirikiane sote tuwe wamoja
(usafi wa mazingira)
Tushirikiane sote tuwe wamoja
(tuyapende mazingira yetu)

Tuyapende mazingira yetu
Tuyatunze mazingira yetu

Written by:
Jessey Jansen

Publisher:
Lyrics © Songtrust Ave

Lyrics powered by Lyric Find

Voice of Maasai

View Profile
Kwata Fagio (feat. Msafiri Zawose & Alex Lobulu) - Single Kwata Fagio (feat. Msafiri Zawose & Alex Lobulu) - Single