Voice of Maasai - Najitazama

Picha linaanza mentali sina kitu mawazo mengi daily
Nakesha nikitafuta aaa a aaa
Na zile ndoto nilizoweka kichwani zishapotea
Mawazo yanitaabisha aaa a aaa
Nikicheki watoto kwangu ni changamoto wangu mama watoto alishakimbia
Kila siku misoto sio baridi ni joto wangu Kulwa na Doto watanifia
Nono nono nono nonooooo/ Wanangu wananiumiza roho ooooo

Juhudi huwa deni kama usipolilipa
Na huwakumbusheni kila inapowaita
Kwenye meno ya tembo usiafiki kabisa
Maana masikini wa upendo hatajiriki na sifa
Kwa sasa ukipata na cha kesho
Chozi utalikata hata bila ya leso
Hata wale wanaoitaka sana pepo
Wananipa mashaka wakipatwa na mateso
Jichunguze kwenye nyuzi nyingi zinazo
Shona uaminifu kwenye maamuzi wanavyo
Lona kama pesa ndo mgunduzi wa liwazo
We kata pumzi uone kama utazikwa nazo

Kila siku nashika tama Kabla ya kufika kesho najitazama
Ona sina dili spesho mi la kufanya
Kila siku miyeyusho tu toka zama
Nono nono nono nonooooo
Wanangu wananiumiza roho ooooo

Verse 3
Ni wengi tu wanajivika ukuu
Fikra ikiwa chini maisha hayawi juu
Kwa mwaka unaahidi harufu ya pilau tu
Kwa kujua eti kila mwaka kuna sikukuu!Ile haraka ya dada kula vya sasa
Ni haraka ya panya kupenda kula vya paka Ile haraka ya kula kuku na bata
Mwisho kula na kaka kabla ya kula talaka Tunapotafuta tujali miiko
Hii safari ya pesa huwa haijali hiko
Na ndomana kuna surgery ya jicho Ila ni ukweli hakunaga daktari wa kifo

Kila siku nashika tama Kabla ya kufika kesho najitazama
Ona sina dili spesho mi la kufanya
Kila siku miyeyusho tu toka zama
Nono nono nono nonooooo
Wanangu wananiumiza roho ooooo

Written by:
Jessey Jansen

Publisher:
Lyrics © Songtrust Ave

Lyrics powered by Lyric Find

Voice of Maasai

View Profile
Najitazama - Single Najitazama - Single